Ukocha ni zaidi ya mbinu za uwanjani.
Ni uwezo wa kujenga timu, kuibua vipaji, kuweka nidhamu na kuwafanya wachezaji kuamini uwezo wao.
Ahmad Ally ni miongoni mwa makocha wazawa ambao wameendelea kuthibitisha uwezo wao katika klabu mbalimbali walizopata nafasi ya kuzifundisha.
Akiwa Prisons, Ahmad Ally aliweza kuibadilisha timu hiyo kutoka katika mfumo wa soka la pira nginja nginja na kuifanya icheze mpira wenye urahisi, mpangilio mzuri na unaovutia mashabiki.
Sasa akiwa na JKT Tanzania, kocha huyo anaendelea kujenga timu yenye ushindani, huku akiwapa nafasi wachezaji kuonyesha uwezo wao na kuifanya JKT Tanzania kuwa moja ya timu ambazo si rahisi kukutana nazo uwanjani.
Uwezo wake wa kujenga kikosi na kuboresha kiwango cha wachezaji unaendelea kumfanya Ahmad Ally kuwa miongoni mwa makocha wazawa wanaotazamwa kwa jicho la karibu katika soka la Tanzania.



