Nasreddine Nabi aachana rasmi na Raja Casablanca

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
1 Sep 2026
Nasreddine Nabi aachana rasmi na Raja Casablanca

Kocha wa Tunisia, Nasreddine Nabi, ameondoka rasmi katika klabu ya Raja Casablanca ya Morocco baada ya wiki kadhaa za mvutano na Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, Rogério Matias.

Mvutano huo ulihusishwa zaidi na sera za usajili, huku Nabi akidaiwa kutoridhishwa na baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu badala ya wale aliowahitaji. Pia kulikuwa na tofauti kuhusu mustakabali wa Badr Benoun, ambaye Nabi alitaka abaki katika kikosi lakini uongozi ulikuwa na mtazamo tofauti.

Nabi kupitia ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii amesema hakuwa na nia ya kuzua mgogoro, akisisitiza kuwa hakuna mchezaji, kocha au mtu binafsi aliye juu ya taasisi. Pia amewashukuru mashabiki wa Raja, akiwemo Ultra Eagles na Green Boys, kwa mapokezi na sapoti waliyompa wakati akiwa klabuni hapo.

Kuondoka kwa Nabi kunaongeza sura nyingine katika mabadiliko ya benchi la ufundi la Raja Casablanca, ikiwa ni kocha wa nane kuondoka tangu klabu hiyo imalize msimu bila taji chini ya Josef Zinnbauer mwaka 2024.

ADVERTISE HERE

More Stories

Ally Kamwe aeleza kuhusu hali ya goli kipa Diarra kuelekea CAFCL
Ally Kamwe aeleza kuhusu hali ya goli kipa Diarra kuelekea CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe afunguka maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya CFFA FC
Ally Kamwe afunguka maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya CFFA FC
1h ago
READ MORE β†’
Infantino aomba radhi kwa utata wa haki za kibiashara FIFA
Infantino aomba radhi kwa utata wa haki za kibiashara FIFA
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yasaka rekodi ya kibabe ligi ya mabingwa
Yanga yasaka rekodi ya kibabe ligi ya mabingwa
2h ago
READ MORE β†’
Kane kuongeza mkataba Bayern Munich hadi 2029
Kane kuongeza mkataba Bayern Munich hadi 2029
2h ago
READ MORE β†’
Reece James afanyiwa upasuaji wa goti
Reece James afanyiwa upasuaji wa goti
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate kurudi Tanzanite Kwaraa, Polisi Tanzania kurejea Ushirika
Fountain Gate kurudi Tanzanite Kwaraa, Polisi Tanzania kurejea Ushirika
7h ago
READ MORE β†’
Beno Kakolanya afunguka sakata la madai ya wachezaji Yanga
Beno Kakolanya afunguka sakata la madai ya wachezaji Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc dimbani Misri kusaka tiketi ya makundi CAFCC
Azam Fc dimbani Misri kusaka tiketi ya makundi CAFCC
7h ago
READ MORE β†’
Didier Drogba kutua Tanzania kuelekea maandalizi ya AFCON 2027
Didier Drogba kutua Tanzania kuelekea maandalizi ya AFCON 2027
7h ago
READ MORE β†’