Mdau wa soka nchini, Edo Kumwembe, amesema Simba SC ilikuwa klabu ya kwanza kuzungumza na mshambuliaji raia wa Namibia, Peter Shalulile kabla ya nyota huyo hatimaye kujiunga na watani wao wa jadi, Yanga SC.
Edo ametoa kauli hiyo kupitia Wasafi, akisema taarifa hizo alizipata kutoka kwa kiongozi wa ndani wa Simba. Kwa mujibu wa maelezo hayo, Simba ilianza mazungumzo na Shalulile huku kocha mkuu wa timu hiyo akipinga usajiri huo kabla ya Yanga kuingia kwenye mchakato na kufanikiwa kumpata mshambuliaji huyo.
Shalulile, ambaye kwa sasa anaitumikia Yanga, ameanza kuonyesha uwezo wake katika Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa tayari amefunga mabao matatu katika msimu huu.



