Afisa Habari wa Gaborone United, Tshepo Molwane, amesema wamejiandaa kwa nguvu kuelekea mchezo wao dhidi ya Young Africans (Yanga SC) katika hatua ya awali ya CAF Champions League.
Molwane amesema tangu walipopata taarifa kwamba watakutana na Yanga, wameanza maandalizi maalum huku wakifuatilia kwa karibu michezo yao ya hivi karibuni ili kuifahamu vizuri timu hiyo.
“Tumekuwa tukijiandaa kwa nguvu sana tangu tumefahamu tutacheza na Yanga SC, tumewafuatilia kwenye michezo yao ya mwisho, tunajua tunaenda kukutana na timu ya aina gani, hautakuwa mchezo mwepesi.”
Kauli hiyo inaonyesha namna Gaborone United inavyolitazama kwa uzito pambano hilo, huku Yanga ikiingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kuanza vizuri safari yake ya kutafuta mafanikio katika michuano ya CAF Champions League msimu huu.



