Winga na kiungo mshambuliaji raia wa Morocco, Hakim Ziyech, amefikia makubaliano ya awali ya kujiunga na Botafogo ya Brazil, akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Wydad Casablanca kwa makubaliano ya pande mbili.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye amewahi kuzitumikia Chelsea na Ajax, anaelekea Brazil kukamilisha taratibu za usajili, ikiwemo vipimo vya afya na kusaini mkataba unaotarajiwa kumweka Botafogo hadi Desemba 2028.
Uhamisho huo unafungua ukurasa mpya katika maisha ya soka ya Ziyech baada ya kipindi kifupi Wydad Casablanca, klabu aliyojiunga nayo Oktoba 2025. Katika kipindi hicho, Ziyech alicheza mechi 16, akifunga mabao tisa na kutoa asisti mbili, huku akikumbana pia na changamoto za majeraha na kutokuwa na mwendelezo wa muda mrefu ndani ya kikosi.