Local, Normal News, Tanzania, Barcelona, Camp nou, Afcon 2027, Kenya, Uganda

Makonda azuru Barcelona, mazungumzo ya maendeleo ya soka Tanzania yatajwa

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
2d ago
Makonda azuru Barcelona, mazungumzo ya maendeleo ya soka Tanzania yatajwa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara maalum nchini Hispania kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya FC Barcelona, akilenga kujadili fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka nchini Tanzania.

Mazungumzo hayo yanahusisha maeneo mbalimbali ya maendeleo ya soka, ikiwemo ukuaji wa vipaji, maendeleo ya kiufundi, uendeshaji wa timu za taifa pamoja na kujifunza uzoefu wa Barcelona katika maandalizi ya mashindano makubwa ya soka. Tanzania ni miongoni mwa wenyeji wa AFCON 2027 pamoja na Kenya na Uganda.

Katika ziara hiyo, Makonda anaambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), huku akitarajiwa pia kushuhudia mchezo wa Barcelona dhidi ya Racing Santander uliopangwa kufanyika Septemba 16, 2026.

Ziara hiyo inalenga pia kufungua fursa za kujifunza na kushirikiana na moja ya klabu kubwa duniani katika maeneo ambayo yanaweza kuchangia maendeleo ya soka la Tanzania, hususan katika malezi ya vipaji, utaalamu wa kiufundi na uendeshaji wa soka.

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →