Chelsea wanatajwa kuwa wanaandaa ofa ya €70 milioni mwezi Januari kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Fabián Ruiz.
Kocha Xabi Alonso anaripotiwa kuwa anamtaka Ruiz, mwenye umri wa miaka 30, aje kuimarisha kikosi cha Chelsea katika dirisha lijalo la usajili.
Hata hivyo, Chelsea watakabiliwa na ushindani kutoka Manchester United, Liverpool, Arsenal na Newcastle United, ambazo pia zimehusishwa na dili la kiungo huyo wa PSG.
Iwapo dili hilo litakamilika kwa thamani ya €70 milioni, Ruiz anaweza kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wanaolengwa na Chelsea katika mipango yao ya Januari.