International, Normal News, Barcelona, Simeone, Raphinha, Lamine Yamal, LA LIGA

Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
1h ago
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone

Kocha wa Atlético Madrid, Diego Simeone, ameipa Barcelona sifa kubwa baada ya timu yake kuifunga Real Madrid mabao 2-1 katika Dabi ya Madrid, akisema kwa mtazamo wake Barcelona ndiyo timu bora zaidi kwa sasa.

Akizungumza na ESPN baada ya mchezo huo, Simeone alisema Barcelona wanaonekana kucheza kwa kiwango tofauti na timu nyingine, huku akivutiwa na mfumo wao wa kushambulia na namna wanavyowapiga presha wapinzani. Kocha huyo alimtaja Raphinha ambaye, kwa mujibu wa kauli yake, tayari amefunga mabao 12 msimu huu, pamoja na Lamine Yamal mwenye mabao saba.

Simeone pia alisifu uwezo wa Barcelona wa kuwapiga presha wapinzani hata wanapocheza nyumbani, akisema wanawanyima muda wa kufanya maamuzi na hawaogopi kuchukua hatari katika mchezo. “Binafsi, naichukulia Barcelona kama timu bora zaidi duniani kwa sasa,” alisema Simeone.

Kauli hiyo imekuja baada ya Atlético kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Madrid Septemba 20. Alejandro Grimaldo alifunga kwa penalti kabla Jonathan David kuongeza la pili, huku Antonio Rüdiger akiifungia Real Madrid bao la kufutia machozi dakika za mwisho. Ushindi huo uliiwezesha Atlético kufikisha pointi 16 na kushika nafasi ya pili, nyuma ya Barcelona.

More Stories

Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
4m ago
READ MORE β†’
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
16h ago
READ MORE β†’
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
17h ago
READ MORE β†’
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
20h ago
READ MORE β†’
Zakaria Thabit afunguka kuhusu mwanzo wa msimu wa Azam FC
Zakaria Thabit afunguka kuhusu mwanzo wa msimu wa Azam FC
20h ago
READ MORE β†’
Kagera Sugar yafukuza benchi zima la ufundi!
Kagera Sugar yafukuza benchi zima la ufundi!
21h ago
READ MORE β†’
Tumejipanga vizuri kukabiliana dhidi ya Kenya AFCON 2027 - Ahmad Ally
Tumejipanga vizuri kukabiliana dhidi ya Kenya AFCON 2027 - Ahmad Ally
23h ago
READ MORE β†’
Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza
Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza
1d ago
READ MORE β†’
Fiston Mayele awasili kambini DR Congo kwa ajili ya kufuzu AFCON 2027
Fiston Mayele awasili kambini DR Congo kwa ajili ya kufuzu AFCON 2027
1d ago
READ MORE β†’