Msemaji wa Simba, Ahmed Ally, amesema wanaamini Simba Marathon ndani ya miaka michache ijayo itakua na kuwa moja ya matukio makubwa ya michezo duniani.
Ahmed Ally amesema maono yao ni kuona Simba Marathon ikifikia hadhi ya matukio makubwa ya kimataifa, akitaja Kombe la Dunia na Michezo ya Olimpiki kama mifano ya matukio yenye mvuto mkubwa duniani.
“Simba Marathon tunaamini, baada ya miaka michache ijayo litakuwa ni tukio kubwa duniani. Ukiachana na Kombe la Dunia, Olimpiki, basi Simba Day ni tukio kubwa, hata Simba Day ni tukio kubwa,” amesema Ahmed Ally.
Kauli hiyo inaonyesha matarajio ya Simba katika kukuza Simba Marathon na kuifanya kuwa sehemu kubwa ya matukio ya michezo yenye kuvuta washiriki na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali.