Kiungo wa ulinzi wa Namungo FC, Kapama maarufu kama Cholo, amesema kuingia kwa Ibrahim Doumbia kipindi cha pili kulikuwa miongoni mwa sababu zilizochangia Simba SC kurejea mchezoni na kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Jumatatu, Novemba 2, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kapama amesema Doumbia alileta mabadiliko makubwa katika mchezo huo kutokana na uwezo wake wa kutuliza na kumiliki mpira, hali iliyosaidia Simba kuongeza kasi ya mashambulizi kipindi cha pili.
Kapama amesema hawezi kusema moja kwa moja nani ni bora kati ya Doumbia na Elie Mpanzu, lakini amesisitiza kuwa Doumbia alikuwa na mchango wa kipekee katika mchezo huo, akimtaja kama mchezaji aliyebadilisha mwenendo wa pambano (game changer).

Doumbia aliingia kipindi cha pili na kuwa sehemu muhimu ya kurejea kwa Simba, baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari na kuipatia timu yake penalti iliyotumiwa na Rushine De Reuck kusawazisha matokeo kuwa 2-2. Baadaye, Anicet Oura alifunga bao la tatu dakika ya 89 na kuipa Simba ushindi wa mabao 3-2.
Kauli ya Kapama inaongeza mjadala kuhusu mchango wa Doumbia katika kikosi cha Simba, hasa baada ya kuonyesha uwezo wa kubadilisha kasi na mwelekeo wa mchezo mara baada ya kuingia akitokea benchi.