Anayetaka kujua ubora wa Yanga aje uwanjani Jumamosi - Samwel

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Anayetaka kujua ubora wa Yanga aje uwanjani Jumamosi - Samwel

Kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, Uongozi wa Klabu ya Yanga umewataka wapenzi na mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani Jumamosi hii ili kujionea wenyewe burudani na ubora wa kikosi chao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Wanachama, Mashabiki, na Masoko wa Yanga SC, Ibrahim Samwel, Jumapili jioni wakati akizungumzia maandalizi ya klabu hiyo kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 10, 2026.

Samwel alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuzindua tawi la Yanga la Kimara Stop Over, ambapo pia alikabidhi rasmi cheti cha Ithibati kwa uongozi wa tawi hilo baada ya kukidhi vigezo vyote vya kuwa tawi rasmi la Yanga.

"Anayetaka kujua ubora wa Yanga aje uwanjani Jumamosi," alisema Samwel kwa kujiamini mbele ya wanachama wa Yanga waliojitokeza kwenye uzinduzi huo, akionyesha imani kubwa aliyonayo kwa kikosi chao kuelekea dabi.

Kumekuwa na maoni hasi kutoka kwa baadhi ya wachambuzi ambao wanaibeza Yanga wakidai ina nafasi ndogo kushinda mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumamosi.

Samwel amesema wako imara na wanaendelea na maandalizi yao ambapo kila idara inatimiza majukumu yake katika kuhakikisha wanaendeleza kile ambacho wamekifanya kwa misimu mitano sasa.

Wito wa kujisajili kidijitali

Aidha, katika hatua nyingine, Samwel alitumia nafasi hiyo kuwaomba na kuwahimiza wapenzi, mashabiki, na wanachama wa Yanga nchi nzima kujitokeza kwa wingi kujisajili ili kuwa wanachama hai wa klabu hiyo.

Alisisitiza kuwa kuwa mwanachama hai ndiyo njia sahihi ya kuunga mkono maendeleo na ustawi wa timu yao kiuchumi na kimuundo.

Yanga SC Stories

Mechi ya mkondo wa kwanza CFFA vs Yanga itapigwa Mauritius
Mechi ya mkondo wa kwanza CFFA vs Yanga itapigwa Mauritius
25m ago
READ MORE β†’
Abuya kuhitimisha majukumu ya Kimataifa leo
Abuya kuhitimisha majukumu ya Kimataifa leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 05 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 05 2026
4h ago
READ MORE β†’
Doumbia amepata chimbo jipya Morocco
Doumbia amepata chimbo jipya Morocco
17h ago
READ MORE β†’
BBD yuko tayari kuendeleza alipoishia
BBD yuko tayari kuendeleza alipoishia
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 04 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 04 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga Princess mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
Yanga Princess mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yajipima na JKT Tanzania Gymkhana
Yanga yajipima na JKT Tanzania Gymkhana
1d ago
READ MORE β†’
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea
2d ago
READ MORE β†’
Yanga Princess kusaka mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
Yanga Princess kusaka mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
2d ago
READ MORE β†’