Meneja ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa mlinda lango namba moja wa timu hiyo Djigui Diarra jana alipata maumivu ya mgongo yaliyopelekea kua chini ya uangalizi wa madaktari.
Kamwe amesema madaktari wameendelea kumuangalia ambapo hatma ya kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA utategemea na ripoti ya mwisho itakayotolewa hapo kesho.
"Maamuzi ya kama Diarra atakosekana au atacheza katika mchezo wa kesho yatategemea majibu ya vipimo na klabu itatoa taarifa rasmi baada ya kuyapata."
"Lakini kama Diarra hatakuwa fiti, Yanga ina makipa wengine wenye uwezo wa kuziba nafasi yake, akiwemo Abuutwalib Mshery na Hussein Masalanga."
"Uwepo wa makipa hawa unatupa matumaini, afya ya Diarra ni muhimu na uamuzi utafanywa baada ya kupata majibu ya madaktari," alisema
Yanga imekamilisha maandalizi yake ya mwisho jioni ya leo katika uwanja wa Azam Complex ambao mchezo huo utapigwa hapo kesho.