FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10h ago
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27

Yanga imelazimika kutoka nyuma kupata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Chrispine Ngushi aliwaadhibu waajiri wake wa zamani Yanga kwa bao la mapema dakika ya 7 lakini Peter Shalulile akairejesha Yanga mchezoni kabla ya mapumziko akimalizia pasi kutoka kwa Stephane Aziz Ki ambaye alirejea kikosini leo baada ya kumaliza adhabu ya kad nyekundu.

Yanga ilitengeneza nafasi nyingi kwenye kipindi cha kwanza lakini ni wazi Mashujaa Fc watamshukuru mlinda lango wao kwa alifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo hatari.

Kipindi cha pili ni kama Wananchi walipunguza kasi huku Mashujaa Fc wakimalisha zaidi eneo lao la ulinzi huku wakitumia mashambulizi ya kushitukiza.

Hata hivyo alikuwa ni Clement Mzize aliyeifungia Yanga bao la ushindi muda mfupi baada ya kuingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Juma Abushir 'Chuga Boy'.

Ni mchezo ambao Yanga ilihitaji ushindi zaidi ili kurejesha morali ya timu baada ya kukosa ushindi katika mechi mbili zilizopita za ligi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’